TANGAZO

ILI KUPATA TAARIFA ZA UHAKIKA KUHUSU MATANGAZO YA KAZI ZA MAENDELEO YA JAMII TEMBELEA BLOG HII KILA MARA Propellerads

Friday, 22 May 2015

NAFASI ZA KAZI AFISA MTENDAJI KIJIJI DARAJA LA III







Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Monduli anawatangazia wananchi wote wenye sifa zilizoanishwa hapa chini kutuma maombi ya kazi kama zilivyotangazwa:-

1.Afisa Mtendaji Kijiji Daraja III - Nafasi 10
Ngazi ya Mshahara TGS B 1

Sifa :

Mwombaji lazima awe amemaliza Elimu ya kidato cha nne (IV) au Sita(VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
Umri: Mwombaji awe na umri kati ya miaka 18 - 40.
Waombaji wote wenye na sifa zilizoainishwa walioajiriwa, wapitishe barua zao kwa waajiri wao, waambatishe nakala za vyeti vya mafunzo, passport size 2 namba ya
simu na CV.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 05/06/2015 saa 9.30 alasiri.

Maombi vote yatumwe kwa;

Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya Monduli,
S. L. P. 1,
MONDULI.
Dominic M. Msagati.
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI (W),
MONDULI

SOURCE; MWANANCHI 20TH MAY 2015

No comments:

Post a Comment