TANGAZO

ILI KUPATA TAARIFA ZA UHAKIKA KUHUSU MATANGAZO YA KAZI ZA MAENDELEO YA JAMII TEMBELEA BLOG HII KILA MARA Propellerads

Friday, 24 April 2015

NAFASI ZA KAZI MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III




Halmashauri ya Mji korogwe kwa mujibu wa muongozo wa katibu mkuu Mkuu Utumishi wa utekelezaji wa maelezo ya serikali kuhusu, Halmashauri kuajiri kwa kumb: Na CCD. 129/215/013 WA TAREHE 9/6/2014, Halmashauri ya Mji korogwe mbali na kuwa na majukumu mengine, inalo jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ngazi ya Halmashauri.

Hivyo inawatangazia watanzania wenye sifa ziliainishwa hapo chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Halmashauri ya mji wa korogwe , kama ifuaavyo:

1, MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III- TGS B (NAFASI 2)
(a) Sifa za kuingilia moja kwa moja
Kuajiriwa mwenyewe Elimu ya kidato cha nne (IV) au sita (VI) aliye hitimu mafunzo ya sistashahada/ cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala , sharia ya jamii, usimamizi wa fedha, maendeleo ya jamii ya sayansi ya sanaa kutoka chuo cha serikali cha serikali za mitaa Hombolo, Dodoma, au chuo chochote kinacho tambuliwa na serikali.

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI

i)Katibu wa kamati ya mtaa
ii) Mtendaji mkuu wa mtaa
iii)Mratibu wa utekelezaji wa sera na sharia zinazotekelezwa na Halmashauri katika mtaa
iv) Mshauri wa kamati ya mtaa kuhusu mipango ya maendeleo katika mtaa
Msimamizi wa utekelezaji mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na umasikini katika
Mtaa.
vi) Mshauri wa kamati ya mtaa kuhusu masuala ya ulinzi na usalama .
vii) Msimamizi wa utekeleaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na umaskini
katika mtaa

Masharti ya mwombaji:

1. Mwombaji awe na umri wa kuanzia miaka 18 hadi 44
2. Mwombaji andike majina yake anayotumia kwa usahili
3. Mwombaji aandike majina yake anayotumia kwa usahili
4. Mwombaji anatatakiwa kuambatanisha nakala ya cheti cha kuzaliwa, vyenye vya elimu/ taaluma na wasifu binafsi (CV)
5. Waombaji watakaokidhi vigezo kuingizwa kwenye orodha ya mapendekezo watajulishwa.
6. Barua za maombi ziandikwe kwa lugha ya kingereza/kiswahli.
7. Waombaji wa kazi wa eneo husika watapewa kipao mbele.
8. Mwombaji ambaye atazingatia maelekezo hapo juu, maombi yake hayatashughulikiwa.
9. Maombi yote yatumwe kwa mkurugenzi wa Mji, Halmashauri ya Mji korogwe, S.L.P 615 korogwe kwa njia ya posta, maombi yatakayo wasilishwa kwanji ya mkono hayatapokelewa.
10. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 4/5/2015

Lewis kalinjuna
Mkurugenzi wa Mji
Halmashauri ya Mji wa Korogwe.

No comments:

Post a Comment