Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega anapenda kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega kuomba nafasi zifuatazo:-
1. MAAFISA WATENDAJL WA VIJIJI III - NAFASI 10
Sifa
• Awe na Elimu ya kidato cha IV au VI
• Awe na AstashahadalCheti katika moja ya fani zifuatazo Utawala au Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na sayansi ya sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma au chuo chochote kinachotambulika na Serikali
• Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 40
Mshahara: Ngazi ya mshahara TGS B sawa na Tshs. 345,000 kwa mwezi.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIWA NA WAOMBAJI WOTE WENYE SIFA NI HAYA YAFUATAYO:
a. Maombi yote yapelekwe/yatumwe kwa; Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya
S,L.P.157
BUSEGA
b. Barua za maombi ziambatane na wasifu binafsi (CV) nakala ya vyeti vya Elimu, taaluma na cheti cha kuzaliwa. Vyeti vyote vithibitishwe na Hakimu au wakili wa Serikali.
c. Asiwe aliacha, kuachishwa au kufukuzwa kazi kwenye Utumishi wa Umma
d. Aambatishe picha moja aliyopiga hivi karibuni (Passport size) na iwe ya rangi
e. Walioajiriwa wapitishe barua zao kwa waajiri wao wa sasa
f. Barua zote ziandikwe kwa mkono zenye anwani ya mwombaji na namba ya simu kama ipo.
g. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 6 Mei, 2015
Imetolewa na
Mkurugenzi Mtendaji wilaya
S,L.P.157
BUSEGA
SOURCE; HABARI LEO 15TH APRIL 2015
No comments:
Post a Comment